Thursday, November 13, 2008

Tovuti

Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wahariri na walimu wakielimishwa kuhusu tovuti na Mwezeshaji kutoka Finland Peik Johansson ambaye hayuko kwenye picha.

‘MTANDAO NI MAMBO YOTE’
Jana ilikuwa ni siku nzuri tena kwa wahariri na walimu kutoka vyuo mbalimbali vya uandishi wa habari wanaoendelea kupata mafunzo kuhusu kompyuta katika Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM) jijini Dar Es Salaam. Tunaishukuru MISA-Tanzania na Mfuko wa kuendeleza vyombo vya habari (VIKES foundation) kwa kuandaa mafunzo ya kompyuta ya siku tano kwa wahariri na walimu. Mwezeshaji alikuwa ni Peik Johansson, mwandishi wa habari kutoka VIKES foundation.

Tuliweza kujifunza changamoto mbalimbali zinazovikabili vyombo vya habari ikiwemo ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuendesha vyombo vya habari, uongozi mbovu na mishahara midogo hali inayosababisha baadhi ya waandishi kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na kukiuka maadili ya kazi yao.

Ili kukabiliana na changamoto hizo Serikali na Taasisi zinapaswa kutafuta wafadhili au kutoa ruzuku kwa vyombo vya habari ili viweze kujiendesha na kufikia malengo iliyojiwekea. Wahariri kwa upande wao wanatakiwa kuhakikisha vichwa vya habari na picha vinawavutia wasomaji na watazamaji ili kuweza kupata soko.

Aidha wamiliki wa vyombo vya habari wanatakiwa kuwaendeleza wafanyakazi wao kielimu ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi ikiwa ni pamoja na kuwalipa mishahara ya kutosha kukithi mahitaji yao ya kila siku kufuatia kupanda kwa gharama za maisha.

Vilevile tuliweza kutembelea tovuti za hapa nchini ikiwemo tovuti ya raia mwema, Daily News, Globalpublisherstz.com, IPPmedia.com, feminahip.co.tz, startvtz.com, citizen.co.tz, parliament.go.tz na majira.co.tz.

Pia tuliweza kutembelea tovuti za waandishi wa habari wa kimataifa mfano CNN.com/world, guardian.co.uk, Daily Nation from Kenya, Mail & Guardian online, IPSnews.net, Africa Journals online, Global voices wiki, Hello in many languages na allAfrica.com.

Hata hivyo tuliweza pia kutembelea tovuti za waandishi mbalimbali wa vitabu kama vile African literature &writers.

Nimejifunza kuwa kupitia mtandao tunaweza kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na safari, hali ya hewa, benki, marais, kusikiliza muziki na miji ya nchi mbalimbali.

Tunatakiwa sisi kama wahariri wa habari kuhakikisha habari zinazoandikwa zinawavutia wasomaji ili tuweze kupata soko ndani na nje ya nchi.

No comments: